Umota wa jumuiya na taasisi za maktaba za kimataifa (IFLA) watuma ujumbe wa shukrani kwa Atabatu Abbasiyya tukufu…

Maoni katika picha
Umoja wa jumuiya na taasisi za maktaba za kimataifa (IFLA Internationl Federation of Library Associations instutions), umetuma ujumbe wa shukrani kwa maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasyya, kupitia ukurasa wake rasmi wa Twita (Twitter), kutokana na Maktaba hiyo kutoa taarifa za maktaba mbalimbali za Iraq na kuifanya Iraq iongezwe katika ramani ya maktaba za kimataifa zilizo chini ya (IFLA), maktaba ya Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya kazi ya kukusanya taarifa za maktaba za Iraq kuanzia kusini hadi kaskazini, baada ya miezi kadhaa ya kufanya kazi hiyo ilikamilika na kukabidhiwa kwa umoja wa jumuiya na taasisi za maktaba za kimataifa kwa ajili ya kuingizwa Iraq katika ramani ya maktaba za duniani (LIBRARY MAP OF THE WORLD).

Baada ya maktaba ya Atabatu Abbasiyya kukamilisha vigezo na masharti ya kushiriki katika kongamano la kimataifa lililo fanyika Kwalalumba mwaka jana, na kukutana moja kwa moja na wahusika wa (WLIC 2018) wanaosimamia ramani ya maktaba duniani, ambapo maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya iliwakilisha nchi ya Iraq katika mkutano wa (LIBRARY MAP OF THE WORLD).

Fahamu kua umoja wa jumuiya na taasisi za maktaba za kimataifa (IFLA) ni taasisi kubwa duniani inayo simamia maktaba na kulinda maslahi ya wanufaika wa maktaba, huchukuliwa kama sauti ya maktaba duniani, inawawakilishi kutoka shilika la UNESCO na wanachama wake wanatoka nchi (150) duniani, ni umoja mkubwa zaidi wa maktaba duniani, pia umoja huo hushiriki katika mkutano wa taaluma wa kimataifa, pia ni mjumbe wa mkutano wa makumbusho kimataifa, na mkutano wa wataalam wa kimataifa, na kamati ya kimataifa ya kukusanya na kusambaza taarifa, pia husaidia kulinda pale maktaba au jambo la kitamaduni linapokua katika hatari.

Kwa taarifa zaidi kuhusu (LIBRARY MAP OF THE WORLD) ingia katika toghuti ifuatayo: https://librarymap.ifla.org/

Na kuangalia wachangiaji rasmi wa ramani ya maktaba ingia katika linki ifuatayo:
https://librarymap.ifla.org/datacontributors/Iraq
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: