Vipengele muhimu alivyo ongea Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya swala ya Ijumaa.

Maoni katika picha
Katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa iliyo swaliwa ndani ya ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s) leo (18 Ramadhani 1440h) sawa na (24 Mei 2019m), chini ya uimamu wa Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai (d.i), Marjaa Dini mkuu ameongelea vipengele vingi vya kimaadili na kijamii, miongoni mwa vipengele hivyo ni:

  • - Mwanaadamu katika maisha ya duniani anatakiwa awe na uhusiano mzuri na ndugu zake pamoja na watu wote katika jamii.
  • - Mwezi wa Ramadhani una umaalumu wake na baraka, nyoyo hulainika na huweza kupokea nasaha na mawaida zaidi kushinda miezi mingine.
  • - Katika maisha tunakutana na changamoto nyingi na tunatofautiana namna ya kukabiliana nazo.
  • - Tunatakiwa kuangalia nafsi zetu, tuchunguze makosa na dhambi zetu kutofanya hivyo husababisha kuanguka na kufeli.
  • - Mwezi wa Ramadhani ni wakati mzuri wa kurekebisha mienendo yetu kushinda miezi mingine.
  • - Miongoni mwa mambo yanayo tishia jamii yetu ni uhasama, mifarakano na kutengana baina ya waislamu.
  • - Uislamu na Maimamu maasumina (a.s) wanataka jamii ya kiislamu yenye nguvu na mshikamano, yenye uwezo wa kupambana na changamoto.
  • - Adui anapoona jamii dhaifu isiyokua na mshikamano huingia na kuivuruga.
  • - Uislamu na Maimamu maasumina (a.s) wanataka jamii ya kiislamu iwe bora kushinda jamii zingine, watu wasome kwetu umoja, mshikamano, kusaidiana, kuhurumiana na tuwe kielelezo cha tabia nzuri.
  • - Uislamu na Maimamu maasumina (a.s) wamekataza kuvunja ungudu na kutengana.
  • - Tumieni fursa ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kuunga undugu baina yenu na kusaidiana wakati wa shida.
  • - Kuunga undugu ni msingi wa kidini na kibinaadamu.
  • - Sio waumini na waislamu peke yao unaotakiwa kuunga nao ungugu bali hata wasiokua waislamu.
  • - Madhara ya kuvunja undugu yanapatikana duniani na akhera kwa jamii ya waislamu au wasio kua waislamu.
  • - Hadithi na riwaya nyingi zinahimiza kuunga undugu.
  • - Baadhi ya hadithi zinasema dhambi ya kuvunja undugu ni kubwa sana baada ya shirki.
  • - Wakati mwingine mtu hushawishiwa na shetani pamoja na jamii na kusababisha awafanyie uovu ndugu zake.
  • - Atakaye vumilia maudhi na ubaya anao fanyiwa na ndugu zake Mwenyezi Mungu atakua msaidizi wake na atamuinua kwa ndugu zake, mbele ya watu na katika jamii kwa ujumla.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: