Habari za Ataba
Khutuba za Ijumaa
15/02/2019
Marjaa Dini mkuu: Mara nyingi watu hawakubali nasaha na kukosolewa huona ni kudharauliwa na kuvunjiwa heshima, hufanya kiburi kwa sababu ya kuikweza nafsi…
Madhumuni muhimu katika khutuba
 • Mara nyingi watu hawakubali nasaha na kukosolewa.
 • Jambo muhimu sana linalo hitajika katika maisha yetu ni utamaduni wa kukubali kukosolewa na kupokea nasaha.
 • Kila mwanadabu –ukitoa maasumu- ni mkosaji, anaweza kufanya vibaya na kufanya madhambi.
 • Kosa linaweza kufanywa na mtu wa aina yeyote, anaweza kua wa kawaida au kiongozi mkubwa katika jamii, pia linaweza kufanywa na mtu mmoja au kundi la watu au jamii fulani.
 • Hadithi inasema: Kila mwanaadamu ni mkosaji na mbora ya wakosaji ni mwenye kutubia.
 • Mwanaadamu amezungukwa na uwezekano wa kufanya makossa kila upande wa maisha yake.
 • Mwanaadamu anatakiwa kuwa makini wakati wote.
 • Hadithi inasema: Mtu asiye hesabu nafsi yake katika kila kitu sio miongoni mwetu.
 • Lazima uangalie mahala na wakati muwafaka wa kumnasihi mtu.
 • Unatakiwa kutumia maneno laini na yasiyo umiza wakati wa kumnasihi mtu.
 • Jitahidi kulinda heshima ya mtu unaye mnasihi.
 • Kila mtu utamnasihi kutokana na namna alivyo.
Marjaa Dini mkuu: Yapasa kurudisha uaminifu tujitahidi isiwe ndoto isi
Marjaa Dini mkuu: Uzushi na upotoshaji wa habari na kuzisambaza bila k
Marjaa Dini mkuu atoa wito wa kuwepo kwa mipaka katika jamii itakayo s
Ziara kwa niaba
Maktaba ya picha za video
Maktaba ya picha za mnato